Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham Hotspur wanaongoza mbio za kumsajili beki wa Manchester City Manuel Akanji, mwenye umri wa miaka 30, wakilenga kuwazidi ujanja AC Milan na Crystal Palace kupata sahihi yake. (Gazetta Dello Sport)
Kocha mkuu wa Barcelona Hansi Flick amesema anaamini kuwa kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22 Fermin Lopez, ambaye ameichezea Hispania mara mbili, hataondoka klabuni hapo katika dirisha hili la usajili licha ya kuhusishwa na Chelsea. (ESPN)
Lakini Chelsea wako tayari kutoa ofa nono kwa ajili ya Lopez, ambaye thamani yake Barcelona ni euro milioni 90 (£78m). (Mundo Deportivo)
West Ham wameingia katika mbio za kumsajili Fabio Vieira kutoka Arsenal, lakini Stuttgart na klabu nyingine kubwa ya Bundesliga pia wanavutiwa na kiungo huyo Mreno mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports Germany)
Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Manchester United na Morocco Noussair Mazraoui, mwenye umri wa miaka 27, anasakwa na klabu ya Serie A, Juventus. (Gazetta Dello Sport – in Italian)
RB Leipzig wanamnyemelea kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya England U21 Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 22, kama mbadala wa Xavi Simons, lakini klabu hiyo ya Ujerumani bado inasita kufikia dau linalohitajika na Liverpool. (ESPN)
Liverpool wanaweza kuhamia kwa kiungo wa Aston Villa na England Morgan Rogers, mwenye umri wa miaka 23, iwapo uhamisho wa Elliott utafanikiwa. (Football Insider)
Winga wa Brazil Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, ataendelea kubaki Real Madrid katika dirisha hili la usajili licha ya klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na Liverpool na Arsenal kuonyesha nia ya kumsajili. (Marca)
Chanzo cha picha, Getty Images
Leeds United bado wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Leicester City na Morocco Bilal El Khannouss, mwenye umri wa miaka 23, baada ya uhamisho wao wa Facundo Buonanotte kutoka Brighton kukwama. (The Athletic)
Chelsea wako tayari kutekeleza kipengele cha mkataba cha kuuzwa kwa mshambuliaji wa Braga Roger Fernandes, mwenye umri wa miaka 19, kabla ya dirisha la usajili wa majira ya kiangazi kufungwa. (A Bola)
Aston Villa wanatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 21.25 kwa ajili ya beki wa kati wa Osasuna na Cameroon Enzo Boyomo, mwenye umri wa miaka 23, huku kocha Unai Emery akitaka kuimarisha safu yake ya ulinzi. (The Telegraph)
Klabu mbili za Ligi Kuu ya England zina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Sevilla na timu ya taifa ya Ubelgiji Dodi Lukebakio, mwenye umri wa miaka 27, huku klabu hiyo ya Hispania ikijiandaa kupokea ofa kabla ya siku ya mwisho ya usajili. (Fabrizio Romano)