Nchini Burundi, Meja Jenerali Bertin Gahungu anashikiliwa na idara za usalama, mamlaka imetangaza. Afisa mkuu wa usalama katika utawala na mkuu wa zamani wa idara ya kijasusi nchini humo, anashtumiwa na mashirika ya haki za binadamu kwa jukumu lake katika ukandamizaji wa maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Nkurunziza mwaka 2015. Kukamatwa katika mazingira yasiyoeleweka, hakujashindwa kuibua hisia.
