
Tangu mwishoni mwa mwezi wa Julai, eneo la Uhispania limeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya wahamiaji haramu wanaowasili katika eneo lake. Miongoni mwao, wale wanajaribu bahati yao kwa kuogelea ni wengi mno.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Casablanca, Matthias Raynal
Eneo la Uhispania la Ceuta linalopatikana kaskazini mwa Morocco, kwa sasa linakabiliwa na ongezeko la wahamiaji wanaowasili kutoka Morocco. Tangu mwishoni mwa mwezi wa Julai, hakuna siku imepita bila watu kadhaa kujaribu kuvuka mpaka kati ya maeneo hayo mawili kinyume cha sheria.
Wakati zaidi ya wahamiaji 1,700 tayari wamewasili Ceuta tangu mwanzoni mwa mwaka, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uhispania, takwimu hii kweli iliongezeka kwa kasi wakati wa wiki mbili za kwanza za mwezi Agosti, na kuingia kinyume cha sheria kwa karibu watu 300 kwenye eneo hilo.
Wakati bahari ni shwari msimu huu wa joto, watu wengi wanajaribu kuogelea ili kufika nchini Uhispania. Ingawa kivuko hicho ni hatari—tangu mwanzo wa mwaka, angalau maiti 21 zimepatikana karibu na Ceuta—wengi sasa wanapendelea kujaribu bahati yao kwa njia hii ili kuepuka kuongezeka kwa udhibiti na uzio wenye ulinzi mkali ambao unasimama kando ya mojawapo ya mipaka miwili tu ya nchi kavu inayotenganisha Afrika na Ulaya.
Majaribio mara nyingi hufanywa kwa makundi, kama vile usiku wa Agosti 15, wakati idadi kubwa ya wahamiaji ilishuhudiwa, wakati watu 300 walijaribu bahati yao kwa kuogelea baharini ili kuhakikisha wameingia Uhispania. Ingawa wengi wao walizuiliwa na vikosi vya usalama vya Morocco na Uhispania Hata kama polisi na maafisa wengi wa idara za usalama wameongeza doria kwenye njia hi, haiwazuii baadji ya wahamiaji kuvuka n kuingia Uhispania.
Matokeo yake, vituo vyote vya wahamiaji huko Ceuta vimejaa kupita kiasi. Katika kituo kilichotengwa kwa ajili ya watoto, kwa mfano, msongamano umezidi 400%.