#HABARI: Jeshi la Polisi Wilaya ya Bariadi, Kikosi cha Usalama Barabarani, limetangaza Oparesheni kuwasaka na kuwachukulia hatua Maafisa Usafirishaji(BODABODA) wanaokiuka Sheria ya matumizi ya vyombo vya usafirishaji kwa kunyofoa baadhi ya vifaa kwenye pikipiki zao ikiwemo Taa, Side Mirrow na namba za usajili wa chombo hicho bila kujali kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa maisha ya watu kwa watumiaji wa barabara.
Oparesheni hiyo imetangazwa na Mkuu wa Usalama Barabarani wa Wilaya ya Bariadi ASP,Yusuph Abdallah.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania