Marekani.  Rapa maarufu, Offset amevunja ukimya kuhusu uvumi unaomhusisha na msanii Saweetie, akikanusha vikali madai kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo huo.

Katika mahojiano maalum na mwigizaji na mtangazaji Keke Palmer, Offset alifunguka kuhusu maisha yake ya ndoa na nyota wa muziki Cardi B, na kuthibitisha kuwa bado mchakato wa talaka yao haujakamilika.

Offset alikiri kwa ujasiri kuwa usaliti wake ndio uliopelekea ndoa yao ya miaka karibu saba kuyumba, akisema amejifunza mengi kutokana na makosa hayo.

OFF 01

“Ni kweli, nilimsaliti Cardi, lakini sio na Saweetie. Hizo ni tetesi tu zisizo na msingi,” alisema Offset huku akionekana kujisogeza kwenye kiti kwa wasiwasi kidogo.

Rapa huyo aliongeza kuwa hana ufahamu juu ya asili ya uvumi huo, akiutaja kuwa “wa ajabu na usio na mantiki.”

Wakati huo huo, Cardi B naye amewahi kufunguka mara kadhaa kuhusu mwenendo wa Offset katika ndoa yao kupitia mitandao ya kijamii, akionyesha wazi kuwa penzi lao limepita changamoto nyingi. Hata hivyo, wawili hao wamekubaliana kwamba kuachana ni hatua bora kwa wote wawili kwa sasa.

Mbali na maisha ya mapenzi, Offset pia alizungumzia kuhusu kumbukumbu za marehemu Takeoff, aliyekuwa mwanachama wa kundi la Migos, pamoja na safari yake ya kuacha kutumia dawa za kulevya aina ya codeine, alizodai zilianza kumlemea baada ya wimbo wao maarufu “Bad & Boujee” kupata mafanikio makubwa.

OFF 02

“Nilikuwa nimepotea kwa muda, lakini sasa nimepata mwelekeo mpya wa maisha,” alisema Offset kwa hisia.

Kwa sasa, Offset anaonekana kuendelea na kazi zake binafsi za muziki, huku mashabiki wakisubiri kuona hatma ya rasmi ya ndoa yake na Cardi B, iliyowahi kuwa moja ya mahusiano maarufu zaidi katika ulimwengu wa muziki wa hip-hop.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *