Hii ni baada ya Rais Andry Rajoelina kuikimbia nchi hiyo.

Katika tangazo alilolitoa kwenye redio ya taifa, Kanali Randrianirina amesema kuwa jeshi limevunja taasisi zote isipokuwa bunge, ambalo limepiga kura ya kumuondoa madarakani Rajoelina.

Ofisi ya rais imepuuzilia mbali maamuzi ya bunge ikisema  kikao cha bunge kilichopiga kura ya kumuondowa madarakani rais Rajoelina kimekosa  uhalali.

Kura hiyo imeungwa mkono na wabunge 130, hiyo ikiwa zaidi ya thuluthi mbilizinazohitajika katika bunge hilo lenye wabnge 163.

Rajoelina ambaye amekataa kuachia ngazi, alisema amekwenda mahali salama kwasababu ya kutishiwa maisha lakini afisa mmoja wa upinzani, chanzo cha kijeshi na mwanadiplomasia mmoja wa kigeni walisema rais huyo mwenye umri wa miaka 51 aliikimbia nchi Jumapili kwa kutumia ndege ya kijeshi ya Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *