Jumuiya ya Afya ya nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC) na Jukwaa la Wabunge wa Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR) wamesaini hati ya makubaliano ya miaka mitano kwa ajili ya kushirikiana katika kutumia jukwaa la wabunge kusukuma ajenda ya afya katika nchi za maziwa makuu.

Wakisaini wakubaliano hayo Dar es salaam Dkt. Ntuli Kapologwe, Mkurugenzi Mkuu ECSA na Dkt Deo Mwapinga Katibu Mkuu (FP-ICGLR) wameeleza ushirikiano huo utahakikisha diplomasia ya afya inaenea, jinsi ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko, upatikanaji wa Chakula kuwa kwa ajili ya kuwa na lishe bora, afya ya uzazi kwa vijana pamoja na Afya ya akili.

Esterbella Malisa ��Mhariri @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *