Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Jacobs Mwambegele amewataka wasimamizi wakuu na wasaidizi, kutenda haki kwenye vituo vya kupigia kura kwa vyama vyote vya siasa, ambavyo vimesimamisha wagombea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano ijayo Oktoba 29, 2025.

Mwambegele ambaye ni Jaji wa Rufaa, amesema hayo leo alipokutana na wasimamizi wakuu pamoja na wasaidizi wa jimbo la Tanganyika mkoani Katavi, ambapo mbali na mambo mengine amewakumbusha kuwa vyama vyote vya siasa nchini viko sawa mbele ya INEC.

Imeandaliwa na Mwanaidi Waziri
Mhariri | @abuuyusuftz

#AzamNews #AzamTVUpdates #UchaguziMkuu2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *