Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin, ameonya kwamba iwapo kutatokea shambulio lolote la Ukraine ndani kabisa ya eneo la Russia, vikosi vya jeshi la nchi hiyo vitatoa jibu la maangamizi.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, amesisitiza maonyo ya Rais wa Russia, Vladimir Putin, akitangaza kwamba shambulio lolote ndani kabisa ya eneo la Russia litakabiliwa na majibu makali.

Peskov amesisitiza kwamba vikosi vya jeshi la Russia viko tayari kwa jibu la haraka na kwamba nchi hiyo haitasalimu amri kwa shinikizo lolote la kigeni, ikiwemo Marekani.

Mapema, wakati wa ziara yake katika kituo cha uongozi wa kijeshi cha Russia, Rais Putin alitangaza mafanikio mafanikio ya jaribio la kombora la Burevestnik la kupiga mabara, silaha yenye uwezo wa nyuklia inayoweza kukwepa mifumo yote ya ulinzi.

Wakati wa ziara yake katika kituo cha mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine, Rais wa Russia amezindua kombora hilo la Burevestnik, ambalo “halina mfano wowote duniani” na linaweza kutumika “dhidi ya maeneo yenye ulinzi mkali popote pale duniani.”

Kombora hilo, ambalo lilifanyiwa jaribio lake la mwisho mwaka wa 2023, linaendeshwa na mtambo wa nyuklia na lina uwezo wa kubeba kichwa cha silaha za atomiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *