Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah wa Namibia jana alimfukuza kazi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Viwanda, Natangwe Ithete.

Ofisi ya Rais wa Namibia ilisema jana kupitia taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba Rais Nandi- Ndaitwah amechukua uamuzi wa kiutendaji na kumuondoa Mheshimiwa Natangwe Ithete katika majukumu yake ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Viwanda, Migodi na Nishati mara moja.” 

Rais wa Namibia sasa atashikilia jukumu la Waziri wa Viwanda, Madini na Nishati lengo likiwa ni kuhakikisha uratibu madhubuti unaendelezwa ndani ya wizara hiyo muhimu. 

Rais Netumba Nandi-Ndaitwah amesema Ithete ataendelea kuwa mbunge licha ya kumfuta kazi. Ndaitwah amesisitiza pia dhamira yake ya kuiona Namibia inakuwa nchi yenye utawala bora, inayowajibika na  kutekeleza ipasavyo vipaumbele vya kitaifa.

Natangwe Ithete amekuwa mbunge wa Namibia tangu mwaka 2015 akikiwakilisha chama tawala cha SWAPO ambacho kinaiongoza Namibia tangu ipate uhuru kutoka kwa mkoloni Mjerumani mwaka 1990. 

Ithete pia alihudumu kama Naibu Waziri wa Fedha wakati wa serikali yai Rais Hage Geingob hadi 2020 na alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi na Uongozi wa Umma kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *