#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Wilson Mwita Charles, mwenye umri wa miaka 53, mkazi wa kitongoji cha Burunga Kata ya Uwanja wa Ndege Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Rhoda Jonathan.
Tarehe 23 Oktoba 2025 majira ya saa 1:00 usiku huko kitongoji cha Burunga Kata ya Uwanja wa Ndege tarafa ya Rogoro Wilaya ya Serengeti, Rhoda Jonathan umri miaka 42, Mkurya, mkulima na mkazi wa kitongoji cha Burunga, aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya mtu/watu kuruka ukuta wa nyumba yake na kutekeleza maauji hayo.
Aidha, baada ya uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Wilson Mwita Charles ambaye ni mume wa marehemu kwa ajili ya mahojiano zaidi juu ya tukio hilo. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia uchunguzi wa tukio hilo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.