Moto wa burudani ya soka ndani ya Kisimbuzi chako cha AzamTV unaendelea wiki hii.
Yanga SC, Simba SC, AzamFC na Singida BS baada ya uwakilishi kimataifa sasa wanarudi nyumbani kwenye NBC Premier League.
Kesho Jumanne, saa 10:00 jioni, Yanga SC watakuwa uwanja wa KMC Complex wakiwakaribisha Mtibwa Sugar.
Alhamis, saa 10:00 jioni, TRA United watakuwa nyumbani dimba la Ali Hassan Mwinyi wakiwaalika Simba SC.
Saa 1:00 usiku, AzamFC watakuwa nyumbani Azam Complex wakikipiga na Singida BS.
Katika Bundesliga, Bayer Leverkusen watakuwa nyumbani Bay Arena wakiwakaribisha mabingwa watetezi FC Bayern Munich.
Kwa kifurushi cha shilingi 28,000 unatazama michezo hii.
#WikiYaMoto #Azamtvsports