
Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amethibitisha jeshi hilo kumkamata mfanyabiashara wa mtandaoni Jenifer Jovin maarufu Niffer.
Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Oktoba 27,2025 baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa mfanyabiashara huyo ametekwa na watu wasiojulikana Sinza jijini Dar es Salaam alipokuwa dukani kwake mapema leo.
“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Oktoba 27,2025 majira ya saa 9 mchana eneo la Sinza Kumekucha, limemkamata na linamuhoji Jenifer Bilikwiza Jovin miaka 26 mkazi wa Masaki Peninsula Kinondoni,” taarifa ya polisi imeeleza
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi hilo, Niffer anashikiliwa kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu katika maeneo mbalimbali jijini kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Kamanda Muliro katika taarifa hiyo ameeleza kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuzingatiwa dhidi ya mtuhumiwa.
Endelea kufuatilia Mwananchi