Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Emanuel Nuwas, amehitimisha rasmi kampeni zake leo, akiahidi kuimarisha sekta muhimu za maendeleo ikiwemo afya, barabara, maji na kilimo.

Amesema atatoa kipaumbele kwa kilimo cha umwagiliaji, hususan katika zao la kitunguu, ili kuongeza uzalishaji, kutoa ajira kwa vijana na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vitakavyowekwa katika kila halmashauri.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *