Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema kuwa amekutana na makundi mbalimbali ya waangalizi wa kimataifa waliofika nchini kufuatilia uchaguzi mkuu na kwamba wamefurahishwa na hali ya utulivu na amani iliyopo nchini wakati taifa likielekea kwenye uchaguzi huo.
Dkt. Samia amesema waangalizi hao wamepongeza Tanzania kwa namna inavyoendesha mchakato wa uchaguzi wake bila dalili za vurugu au uvunjifu wa amani, hali inayodhihirisha ustahimilivu wa kisiasa na ukomavu wa kidemokrasia.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates
