Shirika la Ulinzi wa Raia katika Ukanda wa Gaza umeliambia shirika la habari la AFP leo Jumatano kwamba angalau watu 50, wakiwemo watoto 22, wameuawa katika mashambulizi ya Israel katika eneo la Palestina usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Angalau watu 50 wameuawa, wakiwemo watoto 22 na wanawake na watoto kadhaa, kutokana na mashambulizi ya Israel ambayo yamekuwa yakiendelea tangu jana usiku katika Ukanda wa Gaza,” Mahmoud Bassal, msemaji wa Shirika la Ulinzi wa Raia, ameliambia shirika la habari la AFP Jumatano. 

Watu wengine wapatao 200 wamejeruhiwa katika kile ambacho ni “ukiukaji wa wazi na dhahiri wa makubaliano ya kusitisha mapigano,” ameongeza, akisikitikia hali ya “janga na ya kutisha” katika eneo la Palestina.

Donald Trump asema usitishaji mapigano utadumu licha ya mashambulizi ya Israel

Donald Trump amedai leo Jumatano kwamba mashambulizi ya hivi punde ya Israel katika Ukanda wa Gaza hayajahatarisha usitishaji mpigano na kwamba Israel ilikuwa na wajibu wa kulipiza kisasi kwa shambulio dhidi ya mmoja wa wanajeshi wake.

“Walimuua mwanajeshi wa Israel. Kwa hivyo Israel inalipiza kisasi. Na inapaswa kulipiza kisasi,” rais wa Marekani amesema akiwa ndani ya ndege yake ya irais, Air Force One.

Hamas imekana shambulio lolote dhidi ya wanajeshi wa Israel, ikisema kuwa madai ya Israel ni kisingizio cha mashambulii yake

Mabaki ya hivi punde ya mateka yanahatarisha mapigano, kulingana na Israel

Siku moja baada ya Hamas kurejesha mabaki ya mateka wa Israei, Israel ilidai Jumanne kwamba “mabaki haya ya binadamu” tayari ni ya mateka ambaye alikuwa amekabidhiwa. Na ilishutumu kundi la Hamas…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *