“Tuna uhakika kwamba ikiwa maadui wana chembe ya sababu hawatathubutu kupanga shambulio jipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,” amesema Jumanne hii Muhammad -Reza Aref Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

“Hata hivyo, tunapasa kujiandaa kikamilifu kwa kitendo chochote cha uovu wa adui,” ameongeza Makamu wa Rais wa Iran.

Aref pia ametaja uungaji mkono wa wananchi kama hazina kuu ya serikali na kusisitiza umuhimu wa kulinda umoja na mshikamano wa kitaifa.  Ameashiria vita vya siku 12 vya Israel kwa kushirikiana na Marekani dhidi ya nchi hii mwezi Juni mwaka huu na kusema taifa la Iran liliibuka na ushindi licha ya  upande wa pili kutumia mbinu zake zote, zikiwemo zana za kisasa zaidi za kivita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *