Dar es Salaam. Baadhi ya wanamuziki wakongwe wa Bongo Fleva, wameizungumzia mitandao ya kijamii namna inavyorahisisha kazi zao kuwafikia kwa uharaka mashabiki wao, wakitofautisha na zamani.

Mastaa hao wamezungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti na kikubwa walichokisisitiza ni kutumia kwa akili na siyo mitandao kuwaendesha na mwishowe kufanya vitu vya hovyo katika jamii.

WASA 01

RUTA BUSHOKE

Msanii wa Bongo Fleva, Ruta Bushoke anasema wakati anaanza kufanya kazi hiyo miaka ya 90 hakukuwa na mitandao kama ilivyo kwa sasa, akiamini inawasaidia wasanii kufika mbali.

“Wazazi wetu waliotutangulia walitengeneza njia, tukaja sisi tukaendeleza na wapo wa kizazi hiki wanaoendelea kufanya vizuri, kuhusu namna mitandao inavyotusaidia kwa sasa ni ujumbe gani unapeleka kwa wahusika,” anasema Bushoke na kuongeza;

“Mfano kuna nyimbo zangu za zamani ambazo zinapendwa hadi sasa katika mitandao ya kijamii, mfano Usiende mbali Nami ft Juliana Kanyomozi uliyotoka miaka 12 iliyopita ukipigwa bado una vaibu kubwa.”

WASA 02

JUMA NATURE

“Kwangu imekuwa kazi rahisi kupokelewa katika mitandao hiyo, kwa sababu hata nyimbo zangu za zamani bado zina wafuasi wengi nikimanisha hata hao gen-z, kwa ufupi ukiwa na kazi nzuri ni rahisi kwenda mbali zaidi,” anasema Nature.

WASA 03

Msanii aliyewahi kutamba na wimbo wa Binti Kiziwi, Z Anto anasema:”Japokuwa muda mwingi natumia kufanya vitu vingine, lakini mitandao ya kijamii inarahisisha kazi ya msanii akiwa na nyimbo nzuri, mfano ukiacha wa zamani wapo baadhi wa sasa ambao wametoka kwa kuonekana katika mitandao hiyo.

Anaongeza: “Siyo kwa wanamuziki pekee hata waigizaji kuna ambao kazi zao wanazitoa katika mitandao na wanatoboa mfano nawafuatilia sana wachekeshaji, hivyo ni kutumia akili kujua mitandao inahitaji kitu gani.”

Anasema anaona namna nyimbo zake zinavyofanyiwa chalenji katika mtandao wa Tik Tok, jambo linalomfundisha akifanya kitu kibaya ndivyo kitakavyochukuliwa kwa ukubwa.

WASA 03 (1)

“Mitandao ya kijamii inasaidia kurahisisha kazi ya kupromoti nyimbo, tofauti na zamani ilikuwa ni lazima zipigwe redioni, ila kwa sasa zinaweza zinakaanzia mitandaoni na kwenda redioni na  zikafanya vizuri, jambo lingine nimekuwa nikifanya live bandi naona vaibu la Gen Z wanavyoitikia na kuzipenda,” anasema Linex aliyewahi kutamba na nyimbo kama Moyo wa Subira, Kesho Yangu, Salima ft Diamond Platnumz.

WASA 05

20 PERCENT

“Japokuwa asilimia kubwa ya wasanii wa sasa wanaendekeza kiki, ila naamini muziki ukiwa mzuri unapata mashabiki maana hata nyimbo zangu za zamani naona wanavyozikubali hadi sasa, hivyo inasaidia ila inahitaji akili kuitumia.”

 Miongoni mwa nyimbo zake za sasa zinazopendwa ni Nyumba ya Milele.

Anasema jambo la msingi kwake anazingatia ni vitu gani muhimu ambavyo vitaacha taswila nzuri katika jamii: “Ukitumia vibaya mitandao unaweza kukuta maisha yako ambayo hukutaka dunia ikujue itakujua, kwangu mimi nazingatia muziki wangu uwafikie mashabiki na wapate ujumbe ninaoukusudia.”

Anasema anaona katika mitandao mbalimbali ukiwemo wa Tik Tok watu wanavyofanyia nyimbo zake chalenji:

“Ndiyo maana sitaki kuendeshwa na mitandao zaidi ya kuitumia kwa kazi ili kuendelea kulinda heshima niliyoijenga katika jamii.”

WASA 06

“Nyimbo yangu ya kwanza ya Blur lue nimetoa mwaka 2003 na mitandao haikuwa na nguvu, ukitofautisha na sasa, kitu cha msingi ni namna ya kuitumia ili kupushi muziki, maana hata nyimbo zangu za zamani nikipanda jukwaani bado zinaitikiwa kwa vaibu na mashabiki,” anasema Mr Blue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *