
Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amewafahamisha wajumbe wa Baraza Kuu la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu namna serikali zaidi ya sitini, na hasa madola ya Magharibi na nchi kadhaa za Kiarabu, zimekuwa zikiiwezesha “mashine ya mauaji ya kimbari” ya utawala wa Israel huko Gaza.
Jana Jumanne Bi Francesca Albanese aliwasilisha ripoti yake ya hivi karibuni ambayo toleo lake la mapema lilitolewa chini ya wiki moja iliyopita, kwenye Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Desmond na Leah Tutu, huko Cape Town, Afrika Kusini.
Kkatika ripoti yake hiyo ya kurasa 24, iliyopewa jina la Mauaji ya Kimbari ya Gaza: Jinai za Pamoja, Albanese ameeleza namna mataifa hayo yamekuwa yakifumbia macho mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza huku idadi ya watu milioni mbili na zaidi waliokumbwa na vita na kuzingirwa katika eneo la pwani wakilipuliwa kwa mabomu, wakipoteza maisha kwa njaa na kuangamizwa.
Amesema mtandao mkubwa wa ushirikiano wa kijeshi, uchumi, na kidiplomasia ulianzia Washington na Berlin hadi London na kwingineko.
Albanese ameongeza kuwa mataifa yenye nguvu duniani “yamedhuru, kuasisi, na kuuhami utawala mbaguzi wa kijeshi wa Israel” na kuruhusu mradi wake wa ukoloni wa walowezi kubadilika na kuwa mauaji ya kimbari ” jinai zisizo kikomo dhidi ya wakaziasili wa Palestina.”
Ripoti kurasa 24 ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katiak ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu imeweka wazi namna silaha, teknolojia, na msaada kijasusi kutoka kwa nchi zilizoihami Israel ziilivyousaidia utawala huo kuendeleza mashambulizi ambayo yameacha Gaza ikikabiliwa na njaa na katika maafa.