Nchini Sudan, kiwango cha ukatili unaofanywa na wanajeshi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kinazidi kuwa wazi. Kulingana na ripoti mbalimbali kutoka kwa mashirika ya kibinadamu, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu umefanywa dhidi ya raia maskini, ukiwalenga wakazi wa El-Fasher na wale wanaojaribu kukimbia vurugu, tangu Oktoba 26, tarehe ambayo RSF iliingia katika mji huu wa Kaskazini mwa Darfur, ambao ulikuwa umezingirwa kwa mwaka mmoja na nusu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini Sudan, picha mpya zinathibitisha hofu ya kuongezeka kwa ukatili mkubwa dhidi ya raia. Mnamo Oktoba 28, uratibu wa kamati za upinzani huko El-Fasher ulitangaza rasmi kifo cha askari wa mwisho aliyekuwa akipambania mji huo dhidi ya wanamgambo wa RSF. El-Fasher kwa sasa iko mikononi mwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambavyo, kulingana na serikali ya Khartoum, vinafanya ukatili uliopangwa kwa muda mrefu ambao RSF inaonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

El-Fasher ni vita vinavyoweza kufuatwa kwa kushauriana na vyanzo huria. Video nyingi, zilizoandikwa, kuongozwa, na kusimamiwa na wanachama wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, zinasimulia ugaidi wanaofanya. Mawazo yao yanaonekana kutokuwa na kikomo katika kuunda aina zote za ukatili: watu kunyongwa kwa mikono, watu kuuawa kiholela, na ukatili mwingine ambao ni vigumu kuutazama.

Picha za kutisha

Picha za setilaiti za Maxar zilizosomwa na watafiti katika Chuo Kikuu cha Yale zinaonyesha madimbwi ya rangi nyekundu mbele ya nyumba kadhaa katika vitongoji vya El-Fasher. Nyumba zinapekuliwa moja baada ya nyingine kabla ya kuporwa na kuchomwa moto, kama ilivyo Jumba la Makumbusho la Ali Dinar huko El-Fasher.

Picha zingine zinaonyesha maafisa wa shirika la Hilali Nyekundu wakipigwa, kudhalilishwa, na kutendewa vibaya na RSF. Hatima yao bado haijulikani. Mamia ya watu pia wametekwa nyara, wakiwemo wafanyakazi sita wa afya huko El-Fasher. RSF inadai fidia kutoka kwa familia zao.

Vikosi vya pamoja na jeshi la kawaida vilitangaza mauaji ya raia 2,000 katika mji huo, lakini mnamo Oktoba 28, Jenerali Abou Loulou wa RSF, ambaye jina lake halisi ni Issa Fatef Abdallah Idriss, alijisifu kwa fahari kwenye TikTok kwamba aliwaua raia 2,000 peke yake, na labda zaidi. Kwa furaha anadai yuko tayari kufanya hivyo tena.

Ukatili mkubwa

Ukatili huu mkubwa pia umewalenga watu wa kujitolea waliokuwa wakiwasaidia wakazi wa El-Fasher. Miongoni mwao ni Mohamad Khamis Douda, ambaye tulikuwa tukiwasiliana naye katika RFI, na ambaye alitupa mawasiliano na taarifa kutoka kwa jiji hili lililozingirwa. Tuligundua kwamba aliuawa ghafla, kama mamia ya raia wengine. Kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP huko Tawila, kambi ya wakimbizi iliyoko umbali wa kilomita 60 hivi, raia waliofanikiwa kutoroka “wamejeruhiwa na kuingiliwa na hofu,” na “wanaelezea matukio ya mauaji ya kimbari.”

Wengi wa wale wanaokimbia wanafika Tawila wakiwa wamechoka baada ya kuvumilia vurugu zinazofanywa na FSR. Sylvain Pénicaud, mkurugenzi wa mradi wa Madaktari Wasio na Mipaka, aliwasiliana na RFI katika kambi ya wakimbizi ya Tawila.

Hivi sasa, timu za Madaktari Wasio na Mipaka zinashughulikia wimbi kubwa la watu wanaokimbia El-Fasher.

Mnamo Oktoba 28, Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa aliripoti “mauaji ya kutisha” na “ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana” unaofanywa “na makundi yenye silaha wakati wa mashambulizi.” UNHCR ina wasiwasi kuhusu “kuongezeka kwa ukatili huu” tangu kuanguka kwa jiji hili kutoka mokononi mwa jeshi la serikali, ikisisitiza “hofu kubwa ya familia zilizonusurika siku 500 za kuzingirwa.”

Takriban raia 177,000 bado wako katika jiji hili na iunga vyake, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM); Watu 26,000 wamekimbia mji huo tangu siku ya Jumapili. Maafisa watano wa shirika la Hilali Nyekundu nchini Sudan pia waliuawa wakiwa kazini huko Bara, North Kordofan, na wengine watatu hawajulikani walipo. Mji wa Bara uliangukia mikononi mwa vikosi vya RSF wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *