Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jamhuri ya Niger leo Alkhamisi amebadilishana mawazo na Waziri wa Utalii na Kazi za Mikono wa nchi hiyo kuhusu ushirikiano wa pamoja katika uga wa utalii.

Ali Tiztek, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jamhuri ya Niger amekutana na Sofiane  Aitchata, Waziri wa Utalii na Kazi za Mikono wa nchi hiyo. Katika kikao hicho pande hizo mbili zilijadili na kubadilishana mawazo kuhusu ushirikiano kati ya Iran na Niger katika nyanja za utalii na kazi za mikono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *