Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu wa Kiirani, mauzo ya Iran kwenda Oman yameongezeka kwa asilimia 16.

Tathmini ya hali ya uhusiano wa kibiashara kati ya Iran na Oman katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka 1404 Hijsia Shamsia inaonesha kuwa biashara kati ya nchi hizo mbili ilizidi kuimarika, na kiwango cha mabadilishano ya fedha kilifikia zaidi ya dola bilioni 1.153, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka jana.

Katika kipindi hiki, mauzo ya nje ya Iran yasiyo ya mafuta kwa Oman yaliongezeka kwa asilimia 16 hadi dola milioni 780, na kuchukua nafasi kubwa katika ukuaji wa biashara. Malengo ya biashara ya Iran na Oman katika nusu ya pili ya mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia unachukuliwa kuwa mzuri, na kiwango cha biashara cha kila mwaka kinatarajiwa kuzidi dola bilioni 2.5.

Wakati huo huo, katika miezi sita ya kwanza ya 1404, Hijria Shamsia karibu tani 600 za asali ya asili zilisafirishwa kwenda nchi mbalimbali, na kuiingizia Iran pato la zaidi ya dola milioni mbili. Iraq ndiyo mteja mkubwa zaidi wa bidhaa hii, inanunua asilimia 68 ya asali ya Iran inayouzwa nje. Mauzo yalifanywa kwa Imarati, Pakistan, Malaysia, Iraq, Bahrain, Jordan, Kenya, Qatar, Jamhuri ya Azerbaijan, Kuwait, Tajikistan na Afghanistan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *