
Baada ya uchaguzi wa rais na wabunge uliokumbwa na maandamano na vurugu, hali inaendelea kuwa tete nchini Tanzania siku ya Alhamisi, Oktoba 30, ambapo makabiliano yaliendelea siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa kiuchumi, Dar es Salaam.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kufuatia siku ya uchaguzi iliyokumbwa na maandamano na vurugu, makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yaliendelea siku ya Alhamisi nchini Tanzania. Huko Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi, milio ya risasi iliendelea kusikika katika baadhi ya vitongoji hadi jioni. Mashahidi waliripoti kuwaona maafisa wa polisi wakiwashambulia waandamanaji kwa fimbo na kuwaamuru wakae chini kwenye matope kwa kuwadhalilisha. Kutokana na amri ya kutotoka nje usiku iliyowekwa Jumatano jioni na ambayo bado inaendelea, shule na maduka vimefungwa, na mtu yeyote aliyejaribu kutoka nje alihimizwa na vyombo vya usalama kurudi nyumbani.
Katika hali kama hizo, ni vigumu kupata taarifa zaidi kuhusu hali hiyo. Hasa kwa vile intaneti ambayo ilikuwa umerejeshwa kwa saa chache mapema siku hiyo, ilikatwa tena, anaripoti mwandishi wetu wa habari aliyeko huko Dar es Salaam, Élodie Goulesque. Lakini taarifa chache zinazotolewa zinaonyesha kwamba maandamano na vurugu vimeenea katika miji mingi: Arusha, Kigoma, Mwanza, Songwe…
Huko Arusha, hali pia ilikuwa ya wasiwasi siku ya Alhamisi. Mkazi mmoja ameripoti kusikia milio ya risasi hadi jioni na ana wasiwasi kuhusu kuongezwa kwa muda wa amri ya kutotoka nje. “Hapa, tunaishi kwa shghuli mbalimbali, hasa madereva wa pikipiki za kukodiwa. Hili haliwezi kuendelea kwa muda mrefu zaidi!” anaonya.
“Hali mbaya zaidi ambayo sijawahi kuiona.” Mashahidi wachache walioweza kufikiwa waliripoti kupelekwa kwa vikosi vingi vya usalama. Boniface Mwabukusi, rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) na mtetezi wa haki za binadamu katika mkoa wa Mbeya, kusini magharibi mwa nchi, ameelezea hili kama “machafuko.” “Watu wamepigwa risasi za moto na polisi. Wanawapiga risasi watu wasio na ulinzi, wamekaa mbele ya nyumba zao, au wanatembea mitaani. Watu wamekamatwa, wamepigwa, na hata kuuawa,” amemwambia Liza Fabbian wa kitengo cha RFI kanda ya Afrika. “Nimepitia na kushuhudia chaguzi nyingi, labda nne au tano, na hii ndiyo hali mbaya zaidi ambayo sijawahi kuiona.”
Kulingana na hesabu isiyo rasmi, zaidi ya watu mia moja wameuawa katika siku mbili, na wengine wengi wamejeruhiwa. Serikali bado haijatoa wito wowote wa utulivu, ikirejelea tu ujumbe wake unaohimiza kufanya kazi kwa njia ya video wakiwa nyumbani.
Siku ya Jumatano, katika taarifa kwenye televisheni ya serikali, mkuu wa jeshi, Jacob Mkunda, aliwaita “wahalifu” waandamanaji wanaopinga utawala huo. “Ninawataka wahalifu waachane mara moja na uhalifu wao, vinginevyo vikosi vya ulinzi vitawachukulia hatua za kisheria,” alionya. Hii ilifafanua msimamo wa jeshi, kwani picha zinazoonyesha wanajeshi wakisimama karibu na waandamanaji zilifanya chama cha upinzani cha Chadema kudai siku ya Jumatano kwamba jeshi lilikuwa likilinda maandamano.
Hali kuwa mbaya zaidi
Kwa Boniface Mwabukusi wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika, wimbi hili la hasira halishangazi. “Kuna sababu nyingi za kutoridhika: ukosefu wa ajira, utekaji nyara, watu kutoweka kwa lazima … Yote haya dhidi ya msingi wa kutokujali, na jeshi la polisi ambalo haliwajibiki kwa mtu yeyote. Hii kwa kawaida husababisha raia kuwa na hasira. Vijana wanahisi wamepuuzwa. Wanahisi kwamba nchi yao inauzwa kwa watu wachache. Hiyo ndiyo wanayoilaani katika kaulimbiu zao,” anaelezea.
“Ni kizazi kipya.” Haishangazi kuona vijana hawa kutumia minu zingine. Lakini haya yote yangeweza kuepukwa ikiwa tu wale walio madarakani wangekuwa na msimamo mkali na kukubali mjadala wenye kujenga, mtetezi huyu wa haki za binadamu anasikitika. Lakini hakuna oksijeni iliyobaki. Wamezuia mitandao mbalimbali ya kijamii, Twitter, Facebook … Ndiyo maana watu wameingia mitaani.
