Baada ya kupita miezi kadhaa ya kutochukua hatua, hatimaye serikali ya Lebanon imeamua kupambana na Israel kwa kupeleka jeshi lake mpakani ili kukabiliana na uchokozi wa mara kwa mara wa utawala wa Kizayuni kwenye mipaka yake ya kusini.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars; baada ya kupita miezi kadhaa ya vitendo vya kichokozi vya Israel vya kutoheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano, hatimaye Beirut imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na dola hilo pandikizi.

Nalo Shirika la Habari la Taifa la Lebanon limeripoti habari hiyo kwa kuandika kuwa, jeshi la Lebanon limepeleka vikosi vyake katika mji wa mpakani wa “Mes al-Jabal” wa kusini mwa nchi kwa ajili ya kukabiliana na uvunjifu wa amani na mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na Israel.

Hatua hiyo ya serikali ya Rais Joseph Aoun wa Lebanon imechukuliwa baada ya kuona kuwa Israel inaendelea kukanyaga makubaliano ya kusimamisha vita kwenye mpaka wa kusini mwa Lebanon.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalianza kutekelezwa mwezi Novemba 2024 lakini Israel imekuwa ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo ya kusini mwa Lebanon ikiwa ni kuzidi kuthibitisha kuwa utawala wa Kizayuni ni dola vamizi na pandikizi ambalo kamwe haliheshimu ahadi zake. 

Kabla ya hapo, Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah alikuwa amesisitiza kwamba serikali ya Lebanon ina jukumu la kumtimua adui, kudumisha amani na uhuru na kuzuia uchokozi. Alisema: Tunatoa mwito kwa serikali ya Lebanon kubuni mpango ambao jeshi litaweza kuutumia kukabiliana na uchokozi wa Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *