Nchi saba za Kiislamu, ambazo zimekutana Istanbul siku ya Jumatatu, Novemba 3, kujadili mustakabali wa Gaza, zimesisitiza utawala wa Wapalestina pekee, zikikataa kuwekwa kwa “mfumo mpya wa usimamizi” katika eneo hilo baada ya wiki mbili za usitishaji mapigano dhaifu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Wapalestina lazima watawale ndugu zao Wapalestina, na Wapalestina lazima wahakikishe usalama wao wenyewe,” ametangaza Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, akizungumza peke yake na waandishi wa habari baada ya mkutano na wenzake kutoka Saudi Arabia, Qatar, Falme za Kiarabu, Jordan, Pakistani na Indonesia.

Gaza inahitaji kujengwa upya, na raia wake wanahitaji kurudi nyumbani. Wanahitaji kuponya majeraha ya miaka kadhaa. Lakini … hakuna mtu anayetaka kuona mfumo mpya wa usimamizi ukiibuka,” Fidan amesisitiza. “Hatua yoyote inayochukuliwa kutatua suala la Palestina (…) haipaswi kuhatarisha kuunda msingi wa matatizo mapya. Tunajali sana hili,” alisisitiza, akielezea matumaini yake ya “maridhiano ya haraka kati ya Wapalestina” kati ya Hamas na Mamlaka ya Palestina ya Mahmoud Abbas. Amesema hili, “lingeimarisha uwakilishi wa Palestina ndani ya jumuiya ya kimataifa.”

Recep Tayyip Erdogan akosoa mwenendo “mbaya” wa Israel

Mawaziri wa nchi hizo saba, wote wakiwa wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), walikutana na Donald Trump mwishoni mwa mwezi Septemba huko New York kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kabla ya kuwasilishwa kwa mpango wa amani wa Marekani siku sita baadaye.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya OIC, wakikutana siku ya Jumatatu huko Istanbul, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikosoa mwenendo “mbaya sana” wa Israel tangu usitishaji mapigano kuanza kutumika Oktoba 10, huku akisisitiza kwamba “Hamas inaonekana imeazimia” kuheshimu makubaliano hayo.

“Lazima tutoe msaada zaidi wa kibinadamu kwa watu wa Gaza, na kisha tuanze juhudi za ujenzi upya,” rais Erdogan ameogeza, akitoa wito kwa Jumuiya ya Kiarabu na OIC kuchukua “jukumu la kuongoza” katika suala hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *