Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kusimamisha mapigano nchini Sudan, akisisitiza kwamba moja ya masharti muhimu ya kukomesha vita ni kuzuia silaha mpya kuingia nchini humo, na kusisitiza kwamba kuendelea mtiririko wa silaha kunarefusha mzozo na kuzidisha mateso ya raia.

Guterres amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Doha kando ya Mkutano wa Pili wa Dunia wa Maendeleo ya Jamii kwamba “uhalifu mbaya unaofanywa nchini Sudan hauwezi kuachwa hivihivi na kukwepa adhabu,” akitaka kuanzishwa mifumo halisi ya uwajibikaji ili kuwashtaki wale waliohusika na uhalifu huo, ambao ameutaja kuwa ni ukatili usioweza kupuuzwa.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unafanya kazi kwa uratibu na pande nne, Umoja wa Afrika na IGAD, katika njia inayolenga kuunganisha juhudi za kimataifa na kutoa ujumbe wazi kwa Vikosi vya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RFS) kwamba “vita hivi havikubaliki kabisa, na kwamba umoja na ardhi nzima ya Sudan lazima viheshimiwe katika hali zote.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba pande zote za kimataifa zinafanya kazi kwa lengo moja: kukomesha mapigano mara moja na kusitisha umwagaji damu.

Vita haribu na angamizi vya Sudan vinaendelea huku jamii ya kimataifa ikioonekana kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo wa ndani.

Wakimbizi wa Sudan, El Fasher

Vita hivyo vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa jeshi vilizuka baada ya Jenerali Al Burhan kutaka Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) viwekwe chini ya jeshi la Sudan kufuati mapinduzi ya 2021, suala ambalo lilipiingwa na viongozi wa kikosi hicho. Hadi sasa kumeshafanyika upatanishi mwingi wa kimataifa lakini umeshindwa kutatua mgogoro wa Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *