Nchini Marekani, aliyekuwa Makamu wa rais Dick Cheney amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 84.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Cheney wakati wa uhai wake, alikuwa Makamu wa rais wa rais wa zamani George W Bush, kati ya mwaka 2001 hadi 2009.

Ripoti zinasema, amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa nimonia na matatizo ya moyo.

Atakumbukwa sana kwa kushiriki pakubwa katika kupanga uvamizi wa jeshi  la Marekani nchini Iraq mwaka 2003, baada ya shambulio ya ugaidi la Septemba 11 mwaka 2001.

Cheney wakati wa uhai wake, alikuwa Makamu wa rais wa rais wa zamani George W Bush, kati ya mwaka 2001 hadi 2009.
Cheney wakati wa uhai wake, alikuwa Makamu wa rais wa rais wa zamani George W Bush, kati ya mwaka 2001 hadi 2009. AP – CHARLES DHARAPAK

Wakati hayo yakijiri, wakaazi wa jiji la New York nchini Marekani, wanatarajiwa kumchagua mwanasiasa kijana kutoka chama cha Democratic,  Zohran Mamdani, kuwa Meya mpya, ambaye ni mpinzani wa rais Donald Trump.

Wapiga kura jijini New York wamekuwa wakisema wanamuunga mkono Mamdani mwenye umri wa miaka 34, ambaye pia ana uraia wa Uganda, kwa sababu ni kijana, ana mawazo yanayokubalika na kupambana na gharama ya kupanda kwa maisha, ahadi yake ya kutoa matibabu bila malipo kwa watoto na kuongeza kodi kwa matajiri.

Jiji la New York ndilo kubwa nchini Marekani na mshindi, anatarajiwa kushirikiana kwa karibu na uongozi wa rais Donald Trump, ambaye anamuunga mkono Gavana wa zamani Andrew Cuomo, kushikia nafasi hiyo na hata kutishia kuzuia fedha kwenda New York iwapo mgombea wa Democratic atashinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *