Chanzo cha picha, EPA
Israeli inadhibiti 40% ya jiji la Gaza, msemaji wa jeshi
alisema Alhamisi huku mashambulizi yake yakilazimisha Wapalestina zaidi kutoroka
makazi yao na maelfu ya wengine wakikaidi amri ya Israeli ya kuondoka.
Mamlaka ya Afya ya Gaza ilisema moto wa Israeli kwenye eneo
hilo umewauwa watu wasiopungua 53 siku ya Alhamisi, wengi katika Jiji la Gaza,
ambapo vikosi vya Israeli vimeendelea kusonga mbele kupitia vitongoji vya nje
na sasa viko kilomita chache (maili) tu kutoka katikati mwa jiji.
“Tunaendelea kuharibu miundombinu ya Hamas. Leo
tunashikilia 40% ya eneo la Jiji la Gaza,” msemaji wa jeshi la Israeli
Brigadier Jenerali Effie DeFrin aliambia mkutano wa habari, akitaja vitongoji
vya Zeitoun na Sheikh Radwan. “Operesheni itaendelea kupanuka na
kuongezeka katika siku zijazo.”
“Tutaendelea kuwafuatilia Hamas kila mahali,”
alisema, akiongeza kuwa operesheni hiyo itaisha tu wakati mateka waliosalia wa
Israel watakaporudishwa na utawala wa Hamas kumalizika.
Israel ilianzisha mashambulizi katika mji wa Gaza tarehe
10, Agosti katika kile Netanyahu anasema ni mpango wa kuwashinda wanamgambo wa
Hamas katika eneo la Gaza ambako wanajeshi wa Israeli walipigana vikali zaidi
katika awamu ya kwanza ya vita.
Kampeni hiyo imesababisha ukosoaji wa kimataifa kwa
sababu ya mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo na imezua hali isiyo ya kawaida
ya wasiwasi ndani ya Israeli, ikiwa ni pamoja na mvutano juu ya mkakati kati ya
baadhi ya makamanda wa kijeshi na viongozi wa kisiasa.
Wakaazi walisema Israel ilifanya mashambulizi ya ardhini
na angani katika wilaya za Zeitoun, Sabra, Tuffah na Shejaia za jiji la Gaza.