Kesi dhidi ya rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila, iliyoanza mwezi Julai 2025 mbele ya Mahakama Kuu ya Kijeshi mjini Kinshasa, inakaribia kumalizika. Joseph Kabila Kabange, ambaye aliongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya mwaka 2001 na mapema mwaka 2019 anatuhumiwa kushirikiana na waasi wa M23/AFC. Vyama vya kiraia vimedai makumi ya mabilioni ya dola kama fidia kwa uharibifu uliosababishwa na waasi hao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Mauaji, uporaji, mashambulizi ya silaha, mateso, ubakaji… Rais wa zamani Joseph Kabila anahukumiwa bila kuwepo mahakamani kutokana na uhalifu huu wote unaohusishwa na waasi wa AFC/M23, kundi la waasi ambalo anatuhumiwa kufadhili.

Wanasheria wa vyama vya kiraia wamepinga utambulisho wa Joseph Kabila, ambaye wamemtambulisha kama “raia wa Rwanda,” wakitaka ahukumiwe kwa kosa la ujasusi badala yake. Wameeleza kwa kirefu madhara ya ghasia hizo, wakitaka walipwe fidia kubwa.

Mawakili hao walioteuliwa na serikali wanatafuta karibu dola bilioni 25 kama fidia, huku mikoa ya Kivu Kusini, Ituri na Kivu Kaskazini yakidai nyongeza ya dola bilioni 21 na kutwaliwa kwa mali ya rais huyo wa zamani ilioko katika benki . Mwanasheria mkuu wa jeshi amepanga kuwasilisha hoja zake za mwisho Ileo jumaa saa sita mchana.

Kwa upande wao, ndugu na washirika wa karibu wa Joseph Kabila wanalaani kesi ya kisiasa. Néhémie Mwilanya Wilondja, mkurugenzi wa zamani katika ofisi yake alipkuwa rais, anazungumzia “uhalifu wa serikali” ambapo athari zake “zitakuwa ngumu kupatia suluhu kesho.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *