Tanzania imeelezea ghadhabu yake kwa taarifa zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nje kuwa zilifanywa kwa nia mbaya ya kutaka kuichafulia nchi jina.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Utamaduni Gerson Msigwa aliongeza kuwa taarifa hizo hazikuwa na haki na ni ukiukaji mkubwa.

‘‘Tunapoendelea kusubiri tume ikamilishe kazi yake, kumejitokeza wimbi kubwa la vyombo vya habari hususan vyombo vya habari vya nje kuchapisha na kutangaza taarifa ambazo ni za upande mmoja,’’ alisema Msigwa katika taarifa hiyo. ‘‘Na wakati mwengine kufanya upotoshaji wa taarifa wenye mlengo wa kuchochea chuki kwa Watanzania dhidi ya serikali, kuwagombanisha Watanzania wenyewe kwa wenyewe kutokana na tofauto zao za kisiasa kidini na kikanda,’’ aliongeza.

Msigwa alikuwa anazungumzia taarifa zilizochapishwa wiki hii na CNN pamoja na zingine zilizochapishwa na BBC na wengineo zikionyesha mauaji yanayodaiwa kufanywa wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

CNN iliripoti kuwa zaidi ya watu 2000 waliuawa kufuatia maandamano yaliyopinga matokeo ya uchaguzi mkuu na kuongeza kuwa vyombo vya uslama vilihusika katika kuficha mauaji hayo, japo walisema kuwa juhudi zao za kupata jibu la serikali hazikufua dafu.

Msigwa alikariri kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, punde tu baada ya kuapishwa, ameunda tume maalum kuchunguza madai hayo na watakapo pokea ripoti ndipo watajua muelekeo wa kuchukua kama serikali.

Msigwa aliongeza kuwa Serikali nzima akiwemo Mama Samia Hassan, inasikitishwa na imeumizwa sana na matukio yale na madhara yake na akaviomba vyombo vya habari kushirikiana na serikali na kutoa taarifa zilizokamilika na za haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *