
Malalamiko na hasira za wagombea waliokataliwa katika uchaguzi wa wabunge na serikali za mitaa nchini Gabon wa Septemba 27, 2025, bado hayajasikilizwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Libreville, Yves-Laurent Goma
Siku ya Jumamosi, Agosti 23, Rais Brice Clotaire Oligui Nguema alijibu binafsi katika taarifa iliyosomwa na mmoja wa washauri wake. Kwa hakika aliegemea upande wa wagombea walioenguliwa, ambao wanaituhumu Wizara ya Mambo ya Ndani, inayohusika na kuandaa uchaguzi, kwa uwazi na ukosefu wa haki. “Tabia hizi hazikubaliki,” alisema rais.
Katika taarifa yake, iliyosomwa na mmoja wa washauri wake, Brice Clotaire Oligui Nguema aliitaka serikali yake kifuata na kutekeleza sheria. Rais anashtumu “makosa yasiyokubalika” ambayo “yanadhoofisha usawa wa mchakato wa uchaguzi na kudhoofisha misingi” ya demokrasia ya Gabon.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Nchi wa Gabon, uwazi, haki, na kuheshimu sheria za jamhuri ni jambo lisiloweza kujadiliwa. Kwa hiyo anatoa wito kwa “mamlaka husika kuchukua majukumu yao kwa bidii na bila upendeleo” ili “kuhakikisha uhalali na uaminifu wa demokrasia yetu.”
Akiwa ameidhinishwa na raia wa Gabon wakati wa uchaguzi wa urais wa mwezi Aprili, Brice Clotaire Oligui Nguema alidai kwamba uchaguzi ujao wa wabunge na serikali za mitaa “ufanyike chini ya masharti sawa ya uadilifu, uwazi na amani.” “Tuachane na tabia hii mbovu, isiyojenga,” alisisitiza Mkuu wa Nchi.
Kama ukumbusho, wagombea kadhaa walikataliwa kushiriki kwenye uchaguzi uliopangwa kufanyika Septemba 27, 2025.