Tovuti ya gazeti la kizayuni la Times of Israel imeripoti kuwa, maelfu ya Waisrael wamepanga foleni ndefu mbele ya ubalozi wa Ureno mjini Tel Aviv kwa lengo la kuomba uraia wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, asubuhi mapema siku ya Jumamosi, Waisraeli hao walioenakana wamepanga foleni ndefu mbele ya ubalozi huo kwa ajili ya kuomba uraia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, waombaji waliosimama kwenye foleni iliyoanzia kwenye mlango wa ubalozi hadi eneo la maegesho ya magari chini ya ardhi walikuwa wakisubiri kuomba uraia au kusasisha pasipoti zao za Ureno.

Mwaka 2015, Ureno ilipitisha sheria inayowapa haki ya kuomba uraia wa nchi hiyo Wayahudi wa jamii ya Sephardi walioteswa wakati wa Zama za Usaili katika karne ya 16.

Lakini kutokana na kuwepo idadi kubwa ya maombi, serikali ya Ureno ilitangaza mwaka 2023 kwamba sheria hiyo ilikuwa imeshafikia lengo lake na hivyo kuanzisha utaratibu wenye masharti magumu zaidi.

Tangu utawala wa kizayuni wa Israeli ulipoanzisha vita vya kinyama na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Ghaza mnamo Oktoba 2023, idadi ya Waisraeli wanaotafuta pasipoti ya pili, yaani uraia wa pili imeongezeka.

Makumi ya maelfu ya Waisraeli wamezihama ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel, na shauku ya wazayuni hao kuwa na uraia wa Ureno inaendelea kuongezeka.

Hii ni katika hali ambayo, mbali na kuongezeka wimbi la wazayuni wanaohama na wanaotafuta uraia mwengine, gazeti  Kiebrania la Yedioth Ahronoth liliripoti hivi karibuni kuhusu indhari iliyotolewa na wataalamu wa Israel kwamba, jamii ya kizayuni inakabiliwa na janga kubwa la afya ya akili ambalo wamelielezea kuwa ni “tsunami ya afya ya akili” iliyowaathiri raia wapatao milioni mbili.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, kufuatia matukio ya Oktoba 7, 2023 kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaoomba ushauri na usaidizi wa kisaikolojia, sambamba na kuongezeka kiwango cha uraibu na kudhoofika mafungamano ya kijamii.

Imeelezwa kwamba Israel inakabliwa na maafa ambayo hayajawahi kushuhudiwa ya mripuko wa ugonjwa wa akili wa kiwewe kilichoenea katika jamii, hali mbaya ya watu kupoteza imani sambamba na kuwepo uhaba mkubwa mno wa vituo vya utoaji huduma za tiba ya matatizo hayo…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *