Mapigano yameendelea kupamba moto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku moja Rais Trump wa Marekani kuwaalika viongozi wa Kongo na Rwanda mjini Washington kusaini makubaliano mapya ya amani

Mkataba wa Washington unalenga kuumaliza mzozo wa miongo mitatu katika eneo la mashariki lenye utajiri wa madini. Nchini Kongo kwenyewe, mapigano makali yaliendelea huku kila upande ukiulaumu mwingine.

Muungano wa waasi wa AFC/M23, unaoungwa mkono na Rwanda, ambao uliikamata miji miwili mikubwa mashariki ya Kongo mapema mwaka huu, umesema kupitia msemaji wake Laurence Kanyuka kuwa vikosi tiifu kwa serikali vinafanya mashambulizi. Msemaji wa jeshi la Kongo amesema makabiliano yanaendelea na kwamba vikosi vya Rwanda vinavyatua mabomu.

Rais wa Kongo Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda walithibitisha tena ahadi zao kwa makubaliano yaliyofikiwa mwezi Juni yaliyosimamiwa na Marekani ili kuleta utulivu katika nchi hiyo kubwa na kufungua njia kwa uwekezaji zaidi katika uchimbaji madini wa Magharibi. Wachambuzi hata hivyo wanasema diplomasia ya Marekani ilisitisha kwa muda tu kuongezeka kwa mapigano mashariki ya Kongo lakini ikashindwa kutatua masuala ya kimsingi, ambapo sio Kongo wa Rwanda iliyoweza kutimiza ahadi zilizotolewa katika makubaliano hayo ya Juni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *