Klabu ya soka ya England Arsenal imesema haitoingia mkataba mpya na serikali ya Rwanda mkataba ambao ulikua na lengo la Arsenal kuitangaza Rwanda na kuhamasisha watu kwenda nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali uongozi wa Arsenal umeshinikizwa kutosaini tena makubaliano hayo na washabiki wengi wa Arsenal wakiongozwa na kundi linaloitwa Arsenal for peace.
Kundi hilo na wanachama wengine wa Arsenal wanaamini kuwa kutokana na misimamo yake ya siku nyingi serikali ya Kagame yani Rwanda imekuwa sehemu ya vyanzo vya machafuko mashariki mwa Congo DRC hivyo wao kutangaza nchi hiyo ni kuunga mkono yanayoendelea.
Rwanda imeingia mkataba kama huo pia na PSG ya Ufaransa, na PSG wamesaini kuendelea kuitangaza Rwanda licha ya kukosolewa vikali pia ja baadhi ya wanachama wao.