“Vijana wajiepushe na vurugu na uvunjifu wa amani na shughuli zozote ambazo haziruhusiwi kisheria na vijana wakatae kuhamasishwa kufanya matendo ambayo yanawagharimu wao wenyewe na yanawagharimu nchi yao.
“Vijana watulie wasikilize Serikali yao na watumie fursa zote ambazo Serikali inazipigania au inaziandaa kwa ajili yao. Hatuna muda wa kupoteza kubishana.
“Tutumie nguvu zetu kujenga nchi yetu badala ya kutumia nguvu zetu kubomoa nchi yetu. Tuwe makini na watu ambao wanatutuma kufanya mambo ambayo hatatusaidii na wala hayaisaidii nchi yetu”- @gersonmsigwa, Msemaji wa Serikali.
#Clouds360
#Clouds26Nyoosha
#LainiYaWana