“Watu kuondoka mwezi Desemba kwenda mikoani majumbani kwao imekuwa ni utaratibu unaofanyika kila mwaka na Tarehe ndio hizi na kwenda kusheherekea sherehe za mwisho wa mwaka. Pia natambua kuna hayo maneno kwamba wapo watu wana hofu ya changamoto zilizojitokeza October 29.

Kwa upande wa Serikali tuwahakikishie kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha kwamba watu na mali zao na shughuli zao zinakuwa salama wakati wote na hatutarajii haya maneno yaliyopita hivi karibuni kwamba kinaweza kukatokea vitendo vya vurugu.

“Yamefanyika mazungumzo ya viongozi kuzungumza na makundi ya vijana juu ya athari za kutozingatia sheria. Kichozungumzwa ni kwamba huwenda kukawa na maandamano kesho.

“Mpaka sasa hakuna maombi wala kibali kiliombwa kwa ajili ya maandamano kwa mujibu wa sheria zetu ukifanya maandamano bila kibali unavunja sheria”- @gersonmsigwa, Msemaji wa Serikali.

#Clouds360
#Clouds26Nyoosha
#LainiYaWana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *