Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Saidi Mohamed Mtanda amesema video inayosambaa mitandaoni leo tarehe 09 Desemba 2025 ambayo inaonesha kundi la Wananchi wakitoa maoni yanayosikika yakisema……. β€œNdugu zetu wametekwa sana, Ndugu zetu wameuawa sana na mpaka sasa wengine hawana familia, Watu wamekimbia majumbani mwao wanaishi kama Digidigi, baada ya kuona hilo Watanzania kwa pamoja tukaona tushirikiane tuungane hatumtaki Rais Samia” ni video iliyorekodiwa October 31 na sio leo December 9.

Akizungumza kutoka ofisini kwake RCMtanda amesema kusambazwa kwa video hiyo kumeleta taharuki isiyo ya lazima na amesisitiza kuwa hatua hiyo inaonekana kuwa ya kupotosha na inalenga kuibua wasiwasi miongoni mwa Wananchi hivyo ametoa wito kwa Wakazi wa Mwanza na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hizo za upotoshaji akibainisha kuwa leo hakuna mkusanyiko wowote uliofanyika wala dalili za uvunjifu wa amani katika Jiji.

Cc:-MillardAyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *