
Mwishoni mwa mwezi Novemba, utawala wa rais wa Marekani Donald Trump ulipendekeza mpango wa amani uliokosolewa vikali na Ukraine pamoja na washirika wake wa Ulaya kwa kuwa uliitaka Ukraine kuachia baadhi ya sehemu ya ardhi yake kwa Urusi.
Aidha Zelensky ameongeza kuwa yuko tayari kuandaa uchaguzi mpya nchini Ukraine ikiwa watahakikishiwa usalama huku akisisitiza kuwa Urusi haioneshi nia ya kuendelea na mchakato wa amani , kwani inaendeleza mashambulizi makali dhidi ya miundombinu yake ya nishati.