Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wameanza kufika nyumbani kwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, eneo la Itega jijini Dodoma, kutoa salamu za pole kufuatia kifo chake kilichotokea ghafla asubuhi ya leo.
Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, amesema taifa limepoteza kiongozi aliyekuwa mwema, mchapakazi na mzalendo.
“Ni msiba mkubwa kwa nchi. Mhagama alikuwa mtu wa upendo, aliyeacha alama kubwa katika jamii na kufanya kazi kwa ushirikiano. Atakumbukwa kwa uchapa kazi wake na uadilifu,” amesema Prof. Shemdoe.
@jamesbunuma
#Cloudsdigitalupdate