“Uwepo wa hii mifumo unasaidia. Na huku kutunza takwimu na kuonekana kwa hizi fedha hakuanzii kwenye Taifa kunaanzia kwa mtu mwenyewe. Mtu yoyote ambaye anatumia mifumo ya malipo ana uhakika wa usalama wa fedha zake.
“Ana uhakika wa kuelewa matumizi halisi ya fedha zake na bila kupata upotevu wa hela yoyote. Na hiyo inakwenda mpaka kwenye ngazi ya Taifa mwananchi anapotumia mifumo ya malipo mbalimbali, Serikali inapata usimamizi wa hizo fedha lakini inapata kile ambacho inahitaji kutoka katika matumizi ya mifumo ya malipo”- Fabian Kasole, Meneja Msaidizi, Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa Benki Kuu Ya Tanzania (BoT)
#SentroYaCloudstv