Watu nusu milioni nchini Cameroon wana hatari ya kuachwa bila msaada wa chakula katika wiki zijazo kutokana na uhaba wa fedha, kulingana na shirika la Imoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP). Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linatoa wito kwa wafadhili kukusanya dola milioni 65.5 ili kuendelea kutoa misaada muhimu kwa muda wa miezi sita ijayo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Bila ufadhili huu wa dharura, WFP inasema italazimika kusitisha msaada kwa wakimbizi 240,000 wa Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na wakimbizi wa ndani wa Cameroon mwishoni mwa mwezi Agosti, kusitisha msaada wa lishe kwa zaidi ya watoto 200,000, wajawazito na wanaonyonyesha, na kusitisha usambazaji wa chakula cha shule kwa wanafunzi 60,000.

“Zaidi ya watu nusu milioni wako katika hatari ya kukumbwa na njaa,” anasema Djaousede Madjiangar, afisa wa mawasiliano na msemaji wa ofisi ya kanda ya Mpango wa Chakula Duniani katika Afrika Magharibi na Kati. “Lakini tayari, tunapozungumza, tafiti zetu zimeonyesha kwamba kuna zaidi ya watu milioni mbili, katika makundi yote, walioathirika na njaa kali nchini. Na sababu zinajulikana: migogoro ambayo inazuia watu kufanya shughuli za kilimo, majanga ya tabianchi, na, bila shaka, kupanda kwa gharama ya maisha, na kusababisha kaya karibu kushindwa kupata chakula.”

Ukosefu wa rasilimali za WFP kwa ujumla

Misaada tayari ilibidi kupunguzwa mwezi uliopita kwa wakimbizi wa Nigeria katika kambi ya Minawao Kaskazini mwa Mbali na kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kambi ya Gado katika eneo la Mashariki. “Kuna mama mmoja alituambia kwa mfano kwamba analazimishwa kujinyima chakula, anakataa kula ili watoto wake wapate chakula. Kwa hiyo, familia nyingi zilizoathiriwa zinakosa kula, na wengine wanalazimika kuuza vitu vidogo na vitu vichache walivyobakisha. Hatujui vitadumu kwa muda gani.”

Kupungua kwa jumla kwa rasilimali. Mnamo mwezi wa Julai 2025, WFP ilitoa tahadhari kwa eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kuwakumbusha wafadhili kwamba bila ufadhili, utoaji wa misaada unaweza kuzorota.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *