Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Mhagama umewasili Mjini Songea mkoani Ruvuma, wananchi wamejitokeza kumpokea.
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama, umewasili mkoani Ruvuma huku ukipokelewa na maelfu ya wananchi, viongozi wa serikali, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa na huzuni kubwa kufuatia msiba huo.
Mara baada ya kuwasili, mwili wa marehemu umepelekwa nyumbani kwake katika mtaa wa Makambi, Manispaa ya Songea, kwa ajili ya kuendelea na taratibu na shughuli mbalimbali za mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehee 16/12/2025
#CloudsDigitalUpdetes