Chama cha Waigizaji wa Filamu Mkoa wa Iringa (TDFAA) kimetoa tuzo ya heshima kwa kampuni ya Azam Media Limited kupitia chaneli ya Sinema Zetu HD, ikiwa ni kutambua mchango wa kituo hicho katika kuinua na kuendeleza vipaji vya wasanii wa filamu.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, na kupokewa na mwandishi wa AzamTV mkoani Iringa, Muhammad Nyaulingo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za filamu kwa wasanii wa mkoa wa Iringa.

Chaneli ya Sinema Zetu HD inayopatikana kwa namba 106 kwenye kisimbuzi cha #AzamTV, imeendelea kuwa kielelezo cha juhudi, ubunifu, maarifa na uzalendo kwa kuibua, kukuza na kutangaza kazi za wasanii wa ndani ya nchi.

Imeandaliwa na Mohamed Nyaulingo
Mhariri @abuuyusuftz

#AzamTVUpdates #tuzo #sanaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *