“Kwenye Kikoba, sisi wanawake tunakusanyana pamoja na kupeana elimu ya uwekezaji mdogo wa kuwekeza pesa yetu kidogo kidogo ili baadae tujikwamue kiuchumi sisi na jamii zetu na familia zetu.

Kwa hiyo hata kama baba ataacha hela ndogo pale nyumbani ile ile utaifanyia bajeti ili kidogo uweke akiba na nyingine iendelee na matumizi.

Na tumeenda mbali zaidi sasa hivi wanawake wote tumeelimishana na kupeana majukumu kila mwanamke lazima ajikwamue kiuchumi kwa kufanya shughuli yoyote kwa kuuza karanga, mbogamboga, ili mradi mwisho wa siku lazima ujue kuweka akiba”- Tatu Pokela – Mwanakikoba

#LiveonClouds360
#Clouds26Nyoosha
#LainiYaWana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *