#HABARI: Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na tatu, aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Chanika, wilayani Handeni, mkoani Tanga aliyefahamika kwa jina la Paskal Msekeni, amejinyonga kwa kutumia kamba kwenye dirisha la nyumba yao muda mfupi baada ya kutoka kuangalia luninga na marafiki zake.

Hayo yamebainishwa na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Vailert Geoge, wakati akielezea namna alivyopokea taarifa ya tukio hilo lililoibua maswali kwa ndugu jamaa na marafiki waliohudhuria msiba huo uliopo Mtaa wa Jiweni, Halmashauri ya Mji wa Handeni.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *