
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani jinai zinazoendelea kufanywa na Israel huko Ghaza na mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, na amezitaka nchi za ukanda huu na jamii ya kimataifa ichukue hatua kali za kukabiliana na tishio la mara kwa mara la utawala wa Kizayuni dhidi ya amani na utulivu wa eneo hili na dunia nzima kwa ujumla.
Akigusia mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza kupitia mashambulizi ya kikatili na kuzuia kuingia misaada ya kibinadamu kwenye ukanda huo, Ismail Baghaei, amekumbusha kuwa, jukumu la jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti za kukomesha uhalifu huo na kuwashtaki wahalifu wa kivita na wahusika wa mauaji ya kimbari.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezungumzia pia azimio la hivi karibuni la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ushauri wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo ilisisitizia wajibu wa mataifa yote, kwa mujibu wa Kifungu cha 1 cha Mikataba ya Geneva ya 1949, kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kulaani vikali ukiukwaji wa mara kwa mara na mkubwa wa sheria za kibinadamu na utendakazi wa jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya umati yanayofanywa na utawala wa Kizayuni, na kusisitizia haja ya kukomeshwa kiburi cha utawala wa Kizayuni.
Baghaei amesema kuwa, Marekani na makundi ya Kizayuni wanashirikiana kufanya mauaji ya umati ya Wapalestina na jinai nyingine zinazofanywa na utawala huo pandikizi katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu pamoja na katika nchi za Lebanon na Syria, na amesema: Licha ya kutangazwa madai ya kusitisha mapigano huko Ghaza na Lebanon, lakini utawala wa Kizayuni, kwa msaada kamili wa Marekani na kutojali makubaliano ya kusitisha vita.