#PichaYangSeries Huyu hapa Mzee Maega

Kisa chake kinaanza na maisha yake upande wa Afrika Kusini ambako yeye aliibiwa hazina na mdogo wake Mzee Maige (kwa sasa amefungwa jela).

Alitekwa na kufichwa na Maige kwa miaka mingi kabla ya kuokolewa na watoto wake RADHIA na CHAICHAKA kwa kushirikiana na vyombo vya usalama likiwemo shirika la AIA.

Kwa sasa Maega anaishi na mabinti zake wawili RADHIA na CHAICHAKA ambao tangu utotoni aliwachora ‘tattoo’ migongoni mwao ambazo inaaminika ipo hazina.

Siri ya ramani ipi ndio sahihi anayo yeye mwenyewe Maega aliyezungukwa na wasaliti kulia na kushoto akiwemo mke wake katili Bisura.

Je, mdogo wake Maige anayehangaika na wanasheria ili atoke jela, akitoka itakuwaje? Kumbuka pia Maega ana watesi wengine huko alikokuwa Afrika Kusini, nao wanamuwinda ili wapate hazina aliyoachiwa na wazazi wake.

Tukutane kila Jumatatu hadi Alhamisi kwenye #PichaYangu ya #SinemaZetu saa 1:30 usiku.

#HakikaNiZaKwetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *