Mwaka 2025 haukuwa mzuri sana kwenye mahusiano baina ya wasanii na mashabiki kutokana na yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Oktaba    29, 2025.

Licha ya hayo kuna baadhi ya nyimbo ambazo zimefanya vizuri na zilipokelewa kwa ukubwa na mashabiki wa muziki nchini kuanzia kwenye majukwaa ya kusikilizia muziki ya kidijitali, vyombo vya habari (Radio & Tv), mitandao ya kijamii, pamoja na mitaani.

Zifuatazo ni nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva zilizofanya vizuri mwaka 2025.

Ukiuliza swali kwa mashabiki ni wimbo gani wa Bongo Fleva kwa mwaka 2025 umetikisa kwa kiasi kikubwa? jibu bila kupepesa macho wala kigugumizi watakwambia ni Pawa ya Mbosso.

Hii ni kufuatia mapokezi kuanzia wimbo huo ulipoachiwa ukifanya vizuri kwenye vyombo vya habari majukwaa ya muziki mpaka mtaani.

Wimbo huo ulitoka rasmi Juni 13, 2025, ukiwa ni moja ya nyimbo kutoka kwenye Ep ya Room Number Three ikiwa ni Ep ya kwanza kutoka kwa msanii huyo baada ya kujitoa lebo iliyokuwa ikimsimamia ya Wasafi.

Pawa imejizolea namba za kutosha kwenye majukwaa ya kuuzia na kusikilizia muziki mitandaoni ambapo audio yake ikiwa imesikilizwa mara milioni 7 na video yake ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 51 YouTube.

Rekodi inayoufanya wimbo huo kutazamwa mara nyingi zaidi ya wimbo mwingine wa Bongo Fleva kwenye mtandao huo kwa 2025.

Wimbo huo ambao umetayarishwa na S2kizzy umependwa zaidi kutokana na uandishi wake na melodi kali iliyoimbwa na Mbosso. Hadi sasa Pawa inaremix nne imefanywa na wasanii  mbalimbali Afrika Mashariki

Wimbo wa kwake Dogo Paten akishirikiana na Zuchu, wimbo huo ulikuwa tobo kwa msanii huyo mpya wa singeli na kumfungulia milango katika safari yake ya muziki akipewa tafu iliyosifika na mwanamuziki Zuchu.

Afande haikutawala tu majukwaa ya kuuzia muziki na mitandao ya kijamii bali ulipokelewa kwa ukubwa na mashabiki wengi mtaani na kuonesha mapinduzi ya muziki wa Singeli nchini kwa mwaka 2025.

Wimbo huo uliachiwa rasmi April 26, 2025, ikiwa ni baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichomuonesha Paten akiimba verse yake ndipo msanii Zuchu akavutiwa na wimbo na kuamua kumbariki verse ya mafanikio msani huo chipukizi. Wimbo huo  audio yake imesikilizwa zaidi ya mara milioni 2.4

Wimbo ambao unaiendeleza Combo baina ya wasanii wa Bongo Fleva, Harmonize na Abigail Chams na kuwaweka kuwa miongoni mwa wasanii ambao wameshirikiana kwa ukubwa mwaka 2025 na kazi zikawa na mafanikio makubwa.

Wimbo huo ambao umeimbwa kwa lugha ya Kiingereza ulifanikiwa kuwabamba mashabiki wa Bongo Fleva kutokana na melodi yake kuwa nzuri na uandishi uliyotukuka kutoka kwa wasanii hao ambao walijipachika jina la Grammy Gang.

Me Too ambayo iliachiwa mapema kabisa Februari 27, 2025, audio yake imesikilizwa zaidi ya mara 926k huku video yake ikitazamwa zaidi ya mara milioni 28 katika jukwaa la Youtube.

COPY PASTE

Hii ilikuwa miongoni mwa nyimbo za mwisho kutoka kwa mwanamuziki Ibraah kabla ya kutangaza rasmi amejiengua katika lebo ya Konde Music. Wimbo huo ulipokelewa kwa ukubwa na mashabiki na kuteka mitandao ya kijamii.

Kupitia jukwaa la Youtube video ya wimbo huo imefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 2.

Ya kwake Barnaba akiwa na Diamond Platnumz ilikuwa moja kati ya nyimbo zilizofanya vizuri mwaka 2025.

Audio ya wimbo huo iliachiwa rasmi May 16, 2025, ikiwa imetayarishwa na mtayarishaji mahili wa muziki nchini S2kizzy. Wimbo huo ulisifika kwa uandishi bora na namna ya uimbaji kutoka kwa wakali huo. Audio yake imesikilizwa zaidi ya mara milioni 4.1 huku video yake ikitazamwa zaidi ya mara milioni 26 Youtube.

Ya kwake Mbosso  ikiwa ni nyingine tena kutoka kwenye Ep yake ya Room Number Three. Wimbo huo ambao kwa jina lingine unafahamika kama Bonge la Dada umekuwa mkubwa nchini mara baada tu ya kuachiwa usiku wa kuamkia Juni 13, 2025, na kutumbuizwa kwa mara ya kwanza Mlimanicity Jijini Dar es Salaam.

Wimbo huo ambao bado haujatolewa video yake audio yake imetazamwa zaidi ya mara milioni 6 kwenye mtandao wa YouTube.

 Hatahivyo nyimbo nyingine za Kibongo ambazo zimefanya vizuri kwa mwaka 2025 ni pamoja na Amanda ya kwake Zuchu, ambayo iliachiwa Agosti 1, 2025, ikifanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 13, YouTube, Dunia ya Marioo iliyotoka Agosti 15, 2025, ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 9 Youtube, Tete ya Marioo ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni 35.

Sasampa, Msumari, Nitafanyaje na Nani kutoka kwa Diamond Platnumz. Furaha kutoka kwa Harmonize ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni 30 Youtube.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *