“Kwa upande wa sekta ya maji vision ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwamba tuhakikishe tunamtua mama ndio kichwani. Fedha nyingi sana zimeelekezwa kuweka miundombinu, kusambaza mabomba ya maji yafike kwenye mitaa na vijiji ili wananchi wapate huduma ya maji.
“Pia tumepata miradi ya visima katika maeneo yetu. Vipi visima vimechimbwa kwa ajili ya kusogeza huduma ya maji kwa wananchi. Pia kwa sasa kuna ujenzi wa bwawa la Kidunda ambao tuliuzindua na Leo Mhe. Waziri wa Maji, Juma Aweso pamoja na wakuu wa mikoa walikwenda kutembelea umefika 40% na yote ile ni kuhifadhi maji kipindi cha kiangazi ili maji yaweze kupatikana kwenye wilaya zetu na Jiji letu la Dar es Salaam. Na ndio maana Waziri wa Maji, Juma Aweso halali anapita huku na kule kuhakikisha maji yanapatikana”- @albertomsando, DC Ubungo.
#SentroYaCloudstv
#Clouds26Nyoosha
#LainiYaWana