
Vyanzo vya mahakama vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba washikuwa hao wanashitakiwa kwa “uhalifu, mauaji na kuhatarisha usalama wa taifa”.
Wanajeshi wa ngazi za chini walijitokeza kwenye televisheni ya taifa hilo la Afrika Magharibi mnamo Disemba 7 na kutangaza kumpinduwa Rais Patrice Talon, lakini jaribio hilo lilizimwa haraka na wanajeshi watiifu kwa msaada wa kikosi cha anga cha Nigeria na kikosi maalum cha Ufaransa.
Watu kadhaa waliuawa na hadi sasa kiongozi wa jaribio hilo, Luteni Kanali Pascal Tigri na wanajeshi wengine walioasi hawajapatikana.
Licha ya kusifika kwa kuchochea ukuaji wa uchumi, Rais Talon anatuhumiwa na wakosoaji wake kwa udikteta katika taifa hilo lililowahi kutajwa kuwa mojawapo ya alama za demokrasia.